Huduma za afya Marekani kujadiliwa

Marekani
Maelezo ya picha,

Huduma za afya kujadiliwa nchini Marekani

Bunge la Marekani limepiga kura kuendelea na mjadala wa ama isalie sera ya afya iliyo anzishwa na kumpa heshima kubwa aliyekuwa raisi wa taifa hilo Barrack Obama iondolewe.

Hatua hii inaonekana kama ushindi kwa rais Trump aliye ahidi wakati wa kampeni zake kuiondosha sera hiyo iliyo anzishwa kwa mujibu wa sheria ya huduma kwa gharama rafiki.

Siku za nyuma majaribio kadhaa ya chama cha Republican kuibadilisha sera hii maarufu kwa jina la Obamacare yaligonga mwamba, mara hii kauli ya kuanzisha mjadala ilioibuliwa na kiongozi wa kundi la walio wengi bungeni kabla ya kubainika iwapo ingeungwa mkono vya kutosha na chama cha Republican

Sambamba na hilo la Obamacare, huko Capitol Hill, nyumba ya wawakilishi pia inajiandaa kupiga kura kuiwekea vikwazo vipya Urusi, hatua ambayo tayari imeidhinishwa na baraza la mawaziri ikiwa ni kama kujibu mapigo kwa Urusi kutuhumiwa kuingilia uchaguzi wa Taifa hilo.

Ikulu ya Marekani inasema maamuzi yatafanyika hivi karibuni juu ya hatma ya mwanasheria mkuu wa nchi hiyo Jeff Sessions kwa kushindwa kumchunguza mpinzani wa rais Donald Trump, Bi Hillary Clinton

Aliye kuwa meneja wa kampeni wa Rais Trump,Paul Manfort amekutana na jopo la wapelelezi kujibu maswali juu ya uhusiano na Urusi, na wakati haya yakiendelea msaidizi wa msemaji wa Ikulu Michael Short amejiuzulu.