Libya kusitisha mapigano

Libya
Maelezo ya picha,

Kiongozi wa serikali ya Libya Fayez al-Sarra anayeungwa mkono na umoja wa mataifa

Viongozi wawili mahasimu nchini Libya wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwa lengo la kukuimarisha amani nchini humo

Mazungumzo ya kusitisha mapigano baina ya pande hizo mbili zinazo sigana yaliongozwa na raisi wa Ufaransa Emmanuel Marcon aliyemudu kuwaleta mezani kiongozi wa serikali ya Libya inayoungwa mkono na umoja wa mataifa Fayez al-Sarraj na Khalifa Haftar ambaye ni kiongozi wa kundi linalo jiita Libyan National Army lenye ngome yake mashariki mwa Libya

Ni mara ya kwanza viongozi hao wawili kukubali kuweka sahihi makubaliano ya kuweka silaha chini ,ikiwa ni juhudi za kukabiliana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoikimbia Libya kupitia bahari ya Mediteranian kuelekea bara Ulaya.