Aliyefanya shambulizi kwa msumeno akamatwa na polisi Uswisi

Franz Wrousis hajaeleza kwanini alifanya tukio hilo
Maelezo ya picha,

Franz Wrousis hajaeleza kwanini alifanya tukio hilo

Polisi nchini Uswisi wamasema wamemkata mtu ambaye anaaminika kufanya shambulizi la kwa kutumia msumeno siku ya jumatatu.

Shambulizi hilo lilifanywa ndani ya ofisi moja ya umma.

Baada ya tukio hilo, Franz Wrousis mwenye miaka 51 alimakatwa kilomita 60 nje ya mji wa Schaffhausen, shambulizi hilo lilipotokea.

Maelezo ya picha,

Picha za usalama zikionyesha alivyokuwa akijiandaa na shambulizi hilo

Wafanyakazi watano kwenye ofisi hiyo inayohusika na masuala ya bima ya afya walijeruhiwa vibaya, huku mmoja hali yake ikisemekana kuwa ni mbaya sana.

Mshukiwa huyo alikuwa akifuatiliwa na polisi kabla ya tukio hilo.