Tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia zamfikisha mahakamani Kadinali

Mara zote Kadinali Kadinali George Pell amekana kuhusika na tuhuma hizi
Maelezo ya picha,

Mara zote Kadinali Kadinali George Pell amekana kuhusika na tuhuma hizi

Mmoja wa maofisa wakubwa nchini Vatican Kadinali George Pell amefikishwa mahakamani mjini Melbourne Australia kusikiliza kesi ya unyanyasaji wa kijinsia inayomkabili.

Alipokelewa na vyombo vingi vya habari kutokana na kesi hiyo kuvutia hisia za watu wengi.

Kadinali huyo ambaye amewahi kuhudumu katika miji ya Sydney na Melbourne amekanusha kuhusika katika tuhuma hizo.

Tuhuma za kesi hiyo bado hazijawekwa wazi.

Wachambuzi wanasema kuwa kuhusishwa kwa mtumishi ambaye yupo karibu kuteuliwa na Papa Francis kutashusha heshima yake.