Wapalestina wakataa hatua mpya za Israel mjini Jerusalem

Palestinian Muslim worshippers pray outside Jerusalem's Old City on 25 July 2017

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wapalestina wakataa hatua mpya za Israel mjini Jerusalem

Kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas anasema kuwa ataendelea kukata mawasiliano na Israeli licha ya kuondolewa kwa mitambo ya kutambua chuma eneo takatifu mashariki mwe Jerusalem.

Kuwekwa kwa mitambo hiyo kulisabaisha ghasia mbaya na wapalestina ambao waliiona kama hatua ya Israel kutaka kudhidti eneo hilo.

Israel ilisema kuwa ilikuwa muhimu kuzuia silaha kuingizwa eneo hilo

Inasema kuwa sasa ina mipango ya kuweka kamara za ulinzi.

Pande zote ziko chini ya shinikizo kutoka jamii ya kimataifa kutua mzozo huo katika eneo hilo takatifu ambalo kwa waislamu linalojulikana kama Haram al-Sharif na kwa wayahudi kama Temple Mount.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wapalestina wakataa hatua mpya za Israel mjini Jerusalem

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa eneo la mashariki ya kati, ametaka misukosuko kupungua kabla ya maombi ya Ijumaa ambayo uhudhuriwa na maefu ya watu.

Hatua mpya za usalama zilichukuliwa kufuatia kuuliwa kwa polisi 2 wa Israel.

Licha ya kuongezeka kwa misukusuko, ofisi ya waziri mkuu wa Israel, ilisema Jumanne kuwa itaondoa mitambo ya kutambua chuma na kuweka teknlojia tofauti iliyo bora.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Wapalestina wakataa hatua mpya za Israel mjini Jerusalem

Hatua mpya zitawekwa ndani ya kipindi cha miezi sita inayokuja huku polisi zaidi wakiwekwa hadi wakati huo.

Kulingana na shirika la habari la Reuters watu walionekana wakiondoa mitambo hiyo na kamare zilizowekwa juzi.

Lakini rais wa Palestina Bwana Abbas na kiongozi wa kiislamu ambaye anasimamia eneo hilo takatifu, walitupilia mbali mabadiliko hao wakitaka hali kurejea kawaida.

Maelezo ya picha,

Wapalestina wakataa hatua mpya za Israel mjini Jerusalem