Mwanamke aliyekuwa ametekwa na Boko Haram arudi kwa wapiganaji hao

Aisha Yerima mwenye umri wa miaka 25 alizungumza na Adaobi Tricia Nwaubani Haki miliki ya picha ADAOBI TRICIA NWAUBANI
Image caption Aisha Yerima mwenye umri wa miaka 25 alizungumza na Adaobi Tricia Nwaubani

Mwanamke ambaye alikuwa ametekwa nyara na wapiganaji wa Boko haram amerudi kwa wapiganaji hao kulingana na famialia yake.

Aisha Yerima mwenye umri wa miaka 25 alizungumza na Adaobi Tricia Nwaubani kabla ya kurudi akisema:Sasa nimeona kwamba vitu vyote ambavyo Boko haram walituambia havikuwa vya ukweli.

''Sasa nikisikiza katika redio, nacheka''. Alitoa matamshi hayo baada ya kukamilisha mpango wa kumuondolea itikadi kali, lakini chini ya miezi mitano baadaye aliitoroka familia yake na kurudi kwa wapiganaji hao.

Wakati alipotekwa na wapiganaji hao alikuwa ameolewa na kamanda ambaye alimfurahisha kwa mapenzi ,na kumpa zawadi zenye thamani mbali na kumuimbia nyimbo za mapenzi za kiarabu.

Mwanasaikolojia Fatima Akila ambaye amefanya kazi na mamia ya wanawake waliookolewa anasema kwamba mara nyengine wanaonyesha kuwa na uwezo mkubwa.

''Hawa ni wanawake ambao kwa kipindi kirefu hawakuwa wakifanya kazi, hawakuwa na uwezo, hawakuwa na sauti katika jamii na mara moja wakaanza kuwasimamia kati ya wanawake 30 jadi 100 ambao walikuwa chini ya udhibiti wao''.

Mada zinazohusiana