Maafisa wa kampuni ya mafuta watekwa na Boko Haram Nigeria

Wapiganaji wa Boko haram
Maelezo ya picha,

Wapiganaji wa Boko haram

Kampuni ya mafuta ya Nigeria N-N-P-C, inasema kuwa watafiti 10 wa jiologia, wametekwa nyara na washukiwa wa kundi la Boko Haram

Wanajiolojia hao na masoroveya wa Chuo Kikuu cha Maiduguri, waliviziwa na kutekwa nyara karibu na kijiji cha Jibi kilichoko katika jimbo la Borno, Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Walikuwa wamepewa kandarasi ya kutafuta mafuta karibu na ziwa Chad.

Taarifa nyingine kutoka maeneo hayo, inasema kuwa kuna hofu wameuawa, lakini hilo halijathibitishwa.

Hatahivyo habari za hivi karibuni zimebaini kuwa mmoja ya watafi hao amepatikana.

Msemaji wa NNPC Ndu Ughamadu alithibitisha kwa BBc kwamba Ibrahim Gildado alipatikana akiwa hai lakini hakutoa maelezo zaidi.

Baadhi ya maafisa wa usalama waliokuwa vijana wa kuweka amani mtaani wanaotoka katika eneo hilo pia walipatikana