Makaburi 5 ya watu wenye vipara yafukuliwa Msumbiji

Baadhi ya raia nchini Msumbiji wanaamini kwamba mtu mwenye kipara ana dhahabu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Baadhi ya raia nchini Msumbiji wanaamini kwamba mtu mwenye kipara ana dhahabu

Wakaazi wanaoshi katika wilaya ya kati ya Milange nchini Msumbiji wanasema kuwa miili ya watu watano wenye vipara imefukuliwa katika kipindi cha miezi mitatu kutokana na maswala ya uchawi.

Watu wanaamini kwamba mwili wa mtu mwenye kipara una dhahabu , kulingana na kamanda mmoja wa polisi kwa jina Afonso Dias alieambia BBC mnamo mwezi Juni baada ya misururu ya muaji iliolenga watu wenye vipara.

Wakaazi wa Milange wameitaka serikali kuingilia kati.

Kufikia sasa wakaazi ,na watumiaji wa dawa za kitamaduni pamoja na waliopigania uhuru wamekutana na maafisa wa taasisi ya kitaifa ya urithi na usaidizi wa haki IPAJ.

Mwakilishi wa IPAJ Antonio Gussi aliahidi kuwasilisha malalamishi yao kwa mamlaka husika ,lakini pia akawataka kutokubali tamaduni hizo zilizopitwa na wakati katika siku za usoni.