Mila zinazowabagua pacha magharibi mwa Kenya

Mila zinazowabagua pacha magharibi mwa Kenya

Magharibi mwa Kenya katika jamii ya Wabukusu kungali kuna mila za kuwabagua watoto mapacha na mama wanaowazaa. Majuma machache yaliyopita kuna mzee aliyewafukuza wajukuu wake mapacha waliozaliwa na baadaye wakafariki wakilala katika shamba la mahindi. Muliro Telewa alitembelea Magharibi mwa Kenya katika mji wa Kitale na kuzungumza na Mama Scholastica Wekhuyi anayeeleza masaibu yaliyompata alipowazaa watoto wake ambao wote wana afya na wanafanya vizuri shuleni. Mama Scholastica Wekhuyi.