Maafisa wa kampuni ya mafuta waliotekwa waokolewa Nigeria

Jeshi linafanya oparesheni maalumu sehemu hiyo ambayo kundi la Boko Haram hufanya mashambulizi mara kwa mara
Maelezo ya picha,

Jeshi linafanya oparesheni maalumu sehemu hiyo ambayo kundi la Boko Haram hufanya mashambulizi mara kwa mara

Jeshi la Nigeria limesema kuwa limefanikiwa kuwaokoa wafanyakazi wa kampuni ya mafuta waliokuwa wametekwa na kundi la wapiganaji la Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa mji wa Borno.

Mmoja wa mashuhuda ambaye ni mwananchi anasema alichokiona ni kwamba baadhi ya wafanyakazi hao wameuawa na wengine bado hawajulikani walipo.

Jeshi linasema pia kuwa miili tisa imekutwa katika eneo hilo.

Watekwaji hao walikuwa wamepewa kazi ya kutafuta mafuta karibu na ziwa Chad.