Mwanafunzi mdogo aliyefaulu mtihani wa wanafunzi wakubwa Benin

Peace Delaly Nicoue

Chanzo cha picha, Bob Quenum/BBC

Maelezo ya picha,

Peace Delaly Nicoue

Peace Delaly Nicoue, ndiye mwanafuniz mwenye umri mdogo zaid aliyefanya mtihani wa mwisho unaofahamika kama Baccalaureate nchini Benin mwaka huu na kupata alama za juu.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 11 anasema alifurahishwa baada ya kupata alama 17 kwa 20 katika somo la hesabu.

Huku wanafunzi wengi wakifanya mtihani huo wa mwisho wakiwa na umri wa miaka 18, Peace aliruhusiwa na serikali kuufanya mtihani huo miaka saba kabla ya kuhitimu.

Mwalimu wake anasema kuwa Peace alionyesha mapema dalili za kufanikiwa.

"Akiwa na umiri wa miaka 4 alikuwa akiandika kifaransa na kiingereza bila ya kufanya makosa" alisema mwalimu wake.

Peace anasema kuwa ndoto yake na kusomea nchi inayozungumza lugha ya Kiingereza.