Polisi wakamata wanachama wa dhehebu haramu la Yesu China

Youtube screenshot

Chanzo cha picha, Youbute/Church of the Almighty God

Maelezo ya picha,

Baadhi ya wanachama wa kundi hilo ni maarufu kwa kumpiga mwanamke hadi kufa kwenye duka la McDonald mwaka 2014

Polisi nchini China wamewakamata wanachama 18 wa dhehebu lililopigwa marufukua.

Baadhi ya wanachama wa kundi hilo ni maarufu kwa kumpiga mwanamke hadi kufa kwenye duka la McDonald mwaka 2014, baada ya mwanamke huyo kukataaa kuwapa namba yake ya simu.

Dhehebu hilo linalofahamika kama Church of Almighty God lilianzishwa miaka ya 1990 na linadai kuwa Yesu alirudi duniani kama mwanamke nchini China

Serikali ya China mara kwa mara huvamia madhehebu na kuwakamata wanachama wengi kwa miaka kadhaa.

Wakati wa kuwakamata polisi pia walichukua kompiuta na vitabu vinavyotumiwa na dhehebu hilo.

Imani ya dhehebu hilo ni kuwa Yesu alirudi duniani kama mwanamke.

Mtu pekee anayedai kuwasiliana na mwanamke huyo ni mwalimu wa zamani Zhao Weishan, ambaye alilianzisha miaka 25 iliyopita na sasa ametorokea Marekani.

Maelezo ya picha,

Baadhi ya wanachama wa kundi hilo ni maarufu kwa kumpiga mwanamke hadi kufa kwenye duka la McDonald mwaka 2014