Ni kwa nini Jeshi la Marekani linanunua dawa nyingi za Viagra?

Wanajeshi wa Marekani wanatumia sana dawa za viagra

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Marekani wanatumia sana dawa za viagra

Huku kukiwa na hisia kali kufuatia tamko la rais wa Marekani Donald Trump katika Twitter kwamba watu wanaobadili jinsia hawataruhusiwa katika jeshi la Marekani, takwimu zimeonyesha gharama ndogo ya kiafya miongoni mwa watu wanaobadili jinsia.

Ni kuhusu gharama za fedha zinazotumiwa na jeshi kwa matibabu ya wasio na nguvu za kiume kila mwaka ikiwa ni takriban dola milioni 84 kulingana na gazeti la jeshi.

Shirika linalosimamia maswala ya kijinsia katika jeshi hilo Rand Corporation linakadiria kwamba mwaka huu gharama ya afya ya wanajeshi waliobadili jinsia itaongezeka kwa dola milioni 8.4 kwa mwaka.

Lakini ni kwa nini jeshi la Marekani linagharamika sana kwa kununua dawa za wanaume wasio na nguvu za kiume?

Kwanza Gazeti la jeshi la mwezi februari 2015 liliripoti takwimu zake kutokana na kitengo cha Ulinzi kuhusu afya.

Matumizi ya dola milioni 84.2 yalikuwa ya mwaka huo ,lakini gazeti hilo pia liliripoti kwamba dola milioni 294 zilitumika kununua dawa za Viagra, Cialis na dawa nyengine tangu 2011.

Limeripoti kwamba gharama hiyo inaweza kununua ndege kadhaa za kijeshi.

Mwaka 2014, takriban dawa milioni 1.18 zilitolewa nyingi zikiwa zile za Viagra.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Dawa za Viagra

Lakini zilikuwa za nini?

Ni kweli kwamba baadhi ya dawa hizo zilitumiwa na wanajeshi wasio na tatizo lolote la ukosefu wa nguvu za kiume.

Lakini nyengine nyingi zilitumiwa na watu wengine ikiwemo wanajeshi waliostaafu na wale katika familia za kijeshi

Inajulikana kwamba ukosefu wa nguvu za kiume ni mkubwa miongoni mwa watu wazima hatua inayoelezea gharama kubwa kwa wanajeshi waliostaafu, ambao matibabu yao hulipwa na Tricare, mpango wa afya wa Pentangon kwa wanajeshi.

Chini ya asilimia 10 ya dawa hizo zilitumiwa na maafisa wa jeshi wasio na matatizo yoyote kulingana na ghazeti hilo la jeshi.

Hatahivyo ukosefu wa nguvu za kiume miongoni mwa wale wanaohudumu katika jeshi la Marekani umeongezeka tangu vita vya Iraq na Afghanistan vianze.

Utafiti wa 2014 uliofanywa na kitengo cha afya cha Jeshi ulibaini kwamba visa 100,248 vya ukosefu wa nguvu za kiume vilipatikana miongoni mwa wanajeshi wasio na tatizo lolote kati ya 2004 na 2013 huku kukiwa na viwango vya kila mwaka vikiwa maradufu katika kipindi hicho.

Karibu nusu ya visa vyote vilitokana na maswala ya kisaikolojia kulingana na utafiti.

Utafiti uliofanywa na jarida la matibabu ya uzazi 2015 ulibaini kwamba wanajeshi wa zamani wa kiume walio na matatizo ya kiakili walikuwa na uwezekano mkubwa ikilinganishwa na wenzao kupata tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume ama matatizo mengine ya kingono kulingana na idara inayosimamia wanajeshi wa zamani.

Utafiti mmoja ulisema kuwa asilimia 85 ya wanajeshi wa kiume walio na matatizo ya kiakili waliripoti ukosefu wa nguvu za kiume , ikiwa ni mara nne ya kiwango cha wale wanaotoka vitani ambao hawana matatizo ya nguvu za kiume.

Mwaka 2008 , shirika la Randa Corporation liliripoti kwamba mmoja kati ya wanajeshi watano wa zamani nchini Iraq na Afghanistan walikuwa wakiugua tatizo la kiakili.

Wanajeshi ambao hawakutumwa vitani walionekana kuugua ukosefu wa nguvu za kiume ikilinganishwa na wenzao ambao walitumwa.

Na hatimaye, ukosefu wa nguvu za kiume unahusishwa na magonjwa ya kawaida ikiwemo ule wa moyo, shinikizo la damu na kisukari.

Mwaka 2007, ilikadiriwa kwamba ukosefu wa nguvu za kiume nchini Marekani miongoni mwa wanaume ulikuwa asilimia 18.

Kwa ufupi , ni tatazo la kawaida na wanajeshi wa Marekani hugharamikia matibabu ya mamilioni ya wanajeshi ,ikimaanisha kwamba hutumia Viagra nyingi na dawa kama hizo.

Hatahivyo ,takwimu muhimu kuhusu wanajeshi wasio na matatizo kati ya 2004 na 2013 zinasema kuwa mtu anafaa kuchukua tahadhari wakati anapotazama ushirikiano kati ya vita vya Marekani hivi karibuni, magonjwa ya kiakili na wanaume wasio na nguvu za kiume kwa uhusiano na mataumizi ya juu ya dawa za viagra katika jeshi la Marekani.