Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos amempiku Bill Gates kuwa mtu tajiri zaidi duniani

Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos amempiku Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos amempiku Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani

Mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos amempiku Bill Gates kama mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wenye thamani ya dola bilioni 90.6.

Ongezeko la hisa za Amazon siku ya Alhamisi linamaanisha kwamba thamani ya bwana Bezos imeishinda ile ya mwanzilishi wa Microsoft Bill Gates kulingana na jarida la Forbes.

Bwana Bezos anamiliki mara tano ya hisa hizo ambazo thamani yake imepita dola bilioni 500.

Katika miaka ya hivi karibuni, aliangazia biashara yake ya roketi ya angani ya Blue Origin na gazeti la Washiington Post, ambalo anamiliki.

Vifaa vya kiteknolojia vimeongeza ukuwaji wa thamani za biashara kama vile Bezos na Mwanzilishi wa fecebook Mark Zuckerberg.

Hivi hapa vitu vitano kuhusu bwana Bezos ambavyo ungefaa kuvijua:

  • -Matumizi yake yanaongezeka.

Mapema mwaka huu bwana Bezos alilipa dola milioni 23 kununua eneo la kumbukumbu la kiwanda cha nguo cha zamani mjini washington DC.

Kitakapobadilishwa na kuwa nyumba ya familia, Familia hiyo ya Bezos itakuwa majirani wa Obama pamoja na Ivanka Trump na Mumewe Jared Kushner.

Chanzo cha picha, Mary Evans Picture Library

Maelezo ya picha,

Jumba la Kumbukumbu la kiwanda cha nguo lililopo washington DC

Hivyo ndio vitu ambavyo The washington Post liliripoti, Bwana Bezos alinnunua gazeti hilo 2013 kwa dola milioni 250 fedha zake taslimu.

Familia ya Bezos pia ina nyumba katika mji wa Seattle na Beverly Hills, lakini matumizi ya mali sio swala la kushangaza ikilinganishwa na kile apendacho bwana Bezos ambacho ni sayansi ya angani.

Bwana Bezos anasema kuwa anauza dola bilioni moja ya mali yake katika Amazon kila mwaka ili kufadhili Blue Origin , mradi ambao ameanzisha ili kuanzisha safari za kuelekea angani.

  • -Anapenda ndizi

Ni Bwana Bejos alienzisha mpango wa kuwapatia watu ndizi waliokuwa wakipita kandao kando ya mji wa Amazon mjini Seattle hususana wakati ambapo takriban watu 4,500 huchukua ndizi hizo.

Ijapokuwa yeye na famili ayake wamechangisha fedha nyingi kwa mambo mema, bwana Bezos amekosolewa kwa kutofanya mengi.

Hatoi fedha kwa mashirika yasiotengeza faida kama vile Bill gates , Mark Zuckerberg na wengine wanavyofanya.

Na bado hajajiunga na watu 169 tajiri duniani ambao wameahidi kutoa nusu ya mali yao yote.

Chanzo cha picha, JAMES DUNCAN DAVIDSON / TED

Maelezo ya picha,

Nduguye Mark Bezos amekuwa akifanya kazi za kuwasaidia wasiojiweza

Lakini mwezi uliopita, bwana Bezos alionekana kuwa na wazo.

Alituma ujumbe wa Twitter akiomba mapendekezo kuhusu vile anavyoweza kutoa fedha ambazo zitasaidia ''hapa na pale''.

Inasubiriwa kuonekana ni wazo gani kutoka kuanzisha maktaba na kukuza talanta ya teknolojia barani Afrika miongoni mwa mawazo yake anayolenga kuafikia.

  • -Nduguye ni shujaa

Kusaidia wasiojiweza ndio wazo ambalo nduguye Jeff Mark Bezos

Mnamo mwaka 2011 Marka Bezos anazungumzia kuhusu kujitolea kwake kujiunga na zimamoto kwa mara ya kwanza akisema kuwa alifanya hivyo ili kuonyesha watu jinsi alivyo.

Lakini mtu mwengine aliagizwa kuwa jasiri na kuingia katika nyumba moja iliokuwa ikichomeka kumuokoa mbwa wa mmiliki wa nyumba hiyo..

Mark naye alipewa kazi ya kutafuta viatu vya mmiliki huyo wa nyumba.

Lakini alishukuru sana.

Anajifunza kutoka kwa msemo usemao: iwapo una kitu cha kutoa, ijapokuwa kidogo toa kwa moyo wako wote.Aliwacha kazi ya matangazo ili kufanyia kazi katika kampuni ya kukabiliana na umasikini ya Robin Hood iliopo New York.