Bi Mugabe amtaka mumewe kumtangaza mrithi wake Zimbabwe

Rais Mugabe na mkewe bi Grace Mugabe

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Rais Mugabe na mkewe bi Grace Mugabe

Rais wa Zimbabwe ametakiwa na mkewe kumtaja ''mrithi'' wake ili kupunguza migawanyiko kuhusu mtu atakayemrithi.

''Rais hafai kuwa mwoga kumchagua mrithi wake na neno lake litakuwa la mwisho'',alisema bi Grace Mugabe.

Bwana Mugabe ndio kiongozi mzee zaidi na chama chake cha ZANU PF kimemchagua kuwania urais kwa mara nyengine mwaka ujao.

Lakini makundi pinzani yamekuwa yakiwania urais ili kuimarisha uwezo wao huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya.