Marekani kuchunguza wanajeshi wa Iraq waliotumia nguvu zaidi Mosul

Mmoja wa wanajeshi wa Iraq akiwa amesimama mbele ya majengo yaliyoharibiwa na vita
Maelezo ya picha,

Mmoja wa wanajeshi wa Iraq akiwa amesimama mbele ya majengo yaliyoharibiwa na vita

Jeshi la Marekani limeahidi kuchunguza tuhuma za wanajeshi Iraq waliopo chini ya mafunzo maalumu ya Marekani wanaosemekana kuwa walihusika katika mauaji yaliyopitiliza kwa wapiganaji wa IS mjini Mosul.

Watetezi wa haki za binaadam wanasema kuwa watu kadhaa ambao walidhaniwa kuwa wapiganaji wa IS waliuawa pasipo kuthibitika kama kweli ni wanamgambo ama la.

Wameongeza kuwa miili ya watu ilionekana ikiwa imetapakaa Mosul.

Kwa kipindi kirefu cha vita kati ya wapiganaji wa IS dhidi ya serikali ya Iraq, watetezi wa haki za kibinaadam wamekuwa wakifichua maovu ambayo yalitendeka kinyuma na ilivyokusudiwa.