Macron aitaka Libya kuwakabili wahamiaji haramu kwa kuwapa mahitaji maalum

Mara kwa mara wahamiaji hupitia pwani ya Libya kuingia Ulaya
Maelezo ya picha,

Mara kwa mara wahamiaji hupitia pwani ya Libya kuingia Ulaya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametoa mapendekezo ya kuweka vituo nchini Libya ili kutekeleza mahitaji ya raia wanaomba hifadhi nje ya taifa hilo.

Hatua hiyo ni kufuatia Italia kuonyesha mashaka katika jambo hilo.

Macron amesema kuwa mradi huo utaanza kutekelezwa ndani ya miezi miwili ijayo.

Lakini Waziri mkuu wa Italia ,Paolo Gentiloni, amesema kuwa tatizo la ukimbizi haliwezi kutatuliwa kwa njia ya kuwaondoa nchini humo.

Maelezo ya picha,

Macron anasema hatua hiyo itapunguza ongezeko la wahamiaji haramu Ulaya

Umoja wa jumuiya ya Ulaya inapaswa kuchukua hatua ambazo zitaipatia uwezo Libya kuleta hali ya Amani.

Gentiloni pia amesema kuwa wiki ijayo wanatarajia kuwasilisha muswada bungeni utakaowapa mamlaka Italia kutumia vyombo vya majini kukabiliana na wahalifu ndani ya Libya.