UN: Maelfu ya watu bado wanahitaji misaada Syria

Vikosi vya jeshi la Urusi vikishusha shehena ya chakula Syria
Maelezo ya picha,

Vikosi vya jeshi la Urusi vikishusha shehena ya chakula Syria

Umoja wa mataifa umesema kuwa baada ya nchi za Urusi, Iran na Uturuki kusaidia kupunguza kasi ya mapigano nchini Syria, mamia kwa maelfu ya wananchi wake bado wanahitaji msaada wa haraka.

Mpango wa kuanzisha ukanda maalum ambao utakua unahusika na utoaji misaada hauna maendeleo mazuri.

Maelezo ya picha,

Makovu ya vita

Mkuu wa shirika la kutoa misaada amesema kuwa kwa mwezi huu hakuna msaada uliotolewa kwa sehemu 11 zilizoathirika na vita.

Ameituhumu serikali ya Syria kwa kuzuia misaada ya kibinaadam, huku pia akitaja makundi ya upinzani kwa serikali kama sababu ya kuwarudisha nyuma.