Google kuwapa mafunzo watu milioni 10 barani Afrika

Google kuwapa mafunzo watu milioni 10 barani Afrika

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Google kuwapa mafunzo watu milioni 10 barani Afrika

Google ina mipango ya kuwapa mafunzo watu milioni 10 barani Afrika kuhusu njia za kutumia mitandao katika kipindi cha miaka mitano inayokuja kwa lengo la kuwawezesha kupata ajira.

Msemaji wa kampuni hiyo anasema kuwa, Google pia itawapa mafunzo wahandisi wa mitandaoi 100,000 nchini Nigeria, Kenya na Afrika Kusini.

Mwezi Machi Google ilisema kwa ilikuwa imefikia lengo lake la kuwapa mafunzo watu milioni moja.

Mkurugenzi wa Google Sundar Pichai anasema kuwa kampuni hiyo imejitolea kuwandaa watu wengine milioni 10 kwa ajira siku za usoni katika kipindi cha miaka mitano inayokuja.

Kulingana na Google blog mafunzo hayo yanayotolewa kwa lugha kadha zikiwemo Kiswahili, Hausa na Zulu, na yatahakikisha kuwa asilimia 40 ya watu ambao watapewa mafunzo hayo ni wanawake.