Waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif ajiuzulu baada ya uamuzi wa mahakama

Pakistani Prime Minister Nawaz Sharif arrives in Germany to meet German Chancellor Angela Merkel, 11 November 2014

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pakistan's Supreme Court has recommended an anti-corruption case against Mr Sharif

Waziri mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif amejiuzulu baada ya uamuzi wa mahakama wa kumzuia kushika wadhifa wa serikali kufuatia uchunguzi wa madai ya ufisadi.

Uamuzi huo unakuja baada ya uchunguzi kuhusu utajiri wa familia yake na ufichuzi wa mwaka 2015 wa Panama Papers, uliowahusisha watoto wake na akaunti za benki ugenini.

Bwana Sharif mara kwa mara amekana kufanya lolote baya. Amri hiyo ilitolewa na jopo la majaji watano.

Mahakama ilifurika siku ya Ijumaa na usalama zaidi ukawekwa kwenye mji mkuu, huku maelfu ya wanajeshi na polisi wakitumwa.

Waziri wa mambo ya ndani nchini Pakistan Chaudhry Nisar Ali Khan, alimshauri Bwana Sharif kukubali uamuzi wa leo.

Mahakama imependekeza kufanyika kesi za ufisadi dhidi ya watu kadhaa akiwemo Bwana Sharif, mtoto wake wa kike Maryam na mumewe Safdar, waziri wa fedha Ishaq Dar na wengine kadhaa.

Hakuna waziri mkuu wa Pakistan aliye raia ashawai kumaliza kipindi chake cha miaka mitano.