Ajenti wa Gareth Bale akana madai ya uhamisho wa Manchester United

Gareth Bale kushoto

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Gareth Bale kushoto

Uvumi unaomuhusisha mchezaji wa Real Madrid Gareth Bale na uhamisho ni upuzi na ujinga kulingana na ajenti wa mchezaji huyo.

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kuwa hawezi kuhakikisha kuwa Bale ,Cristiano Ronaldo na Karim Benzema watasalia katika uwanja wa Bernabeu.

Hatua hiyo imezua ripoti kwamba Manchester United huenda ikafufua hamu yao ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa miaka 28.

Ni habari ya ujinga na kijinga" ajenti Jonathan Barnett aliambia BBC Sport.

Bale alikumbwa na majeraha msimu uliopita na kupoteza nafasi yake kwa Isco, lakini akaimarika chini ya uongozi wa Zidane na kuzawadiwa nafasi moja miongoni mwa 30 za wanaowania tuzo la Ballon d'Or.

Hatahivyo huku Real ikihusishwa na uhamisho wa kitta cha pauni 180 kumnunua mshambulikaji Kylian Mbappe , kumekuwa na ripoti kwamba watalazimika kumuuza mmojawapo wa Bale, Ronaldo ama Benzema.

Alipulizwa kuhusu watatu hao siku ya Alhamisi, Zidane alisema:Nataka kila mmoja aliyepo hapa kusalia lakini chochote chaweza tokea kabla ya Agosti 31.