Uchaguzi Kenya: Habari bandia za BBC na CNN zasambazwa

Habari bandia kuhusu uchaguzi wa Kenya zasambazwa
Image caption Habari bandia kuhusu uchaguzi wa Kenya zasambazwa

Ripoti ya habari bandia kuhusu uchaguzi wa Kenya ambayo imetengezwa kuonesha kana kwamba inatoka katika chombo cha habari cha CNN imekuwa ikisambazwa katika mitandao ya kijamii.

Inajiri baada kanda bandia ya video ikiigiza kipindi cha BBC Focus Africa ilisambazwa katika mitandao ya kijamii siku ya Ijumaa.

Video zote mbili zilikuwa na uongo uliokuwa ukionyesha rais Uhuru Kenyatta akiongoza katika kura za maoni kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa mwezi Agosti.

Ukweli ni kwamba kura za maoni za hivi karibuni zinaonyesha kuwa viongozi wakuu katika uchaguzi huo Rais Uhuru Kenyatta na raila Odinga wa NASA hakuna mgombea anayeweza kushinda moja kwa moja.

Utafiti wa hivi majuzi unaonyesha kuwa asilimia 90 ya Wakanenya wameona ama hata kusiki habari bandia kabla ya uchaguzi huo.

CNN imeenda katika mtandao wa Twitter kuthibitisha kwamba video hiyo ni feki , huku BBC ikiwataka wananchi kuthibitisha habari zozote kwamba zinatoka BBC kupitia kutembelea mtandao wa idhaa hii.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Video zote mbili zilikuwa na uongo uliokuwa ukionyesha rais Uhuru Kenyatta akiongoza katika kura za maoni kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa mwezi Agosti.

Uchaguzi huo kwa mara nyengine utawashirikisha rais Uhuru Kenyatta dhidi ya wagombea wengine saba wakiongozwa na Raila Odinga .

Ili kuweza kushinda moja kwa moja, mgombea ni sharti kupata asilimia 50 ya kura pamoja na kura moja.

Mbali na takriban asilimia 25 ya kura katika nusu ya kaunti 47.

Iwapo hakuna mtu atakayefikisha kiwango hicho kura hiyo itapigwa kwa awamu ya pili.

Kura za maoni za hivi karibuni zimeonyesha matokeo yanayokanganya kuhusu iwapo Raila Odinga anaongoza ama Uhuru Kenyatta.

Mada zinazohusiana