Afisa wa kampuni ya Acacia azuiliwa kwa muda Tanzania

Kisa hicho kinafuatia shinikizo za serikali kwa wafanyikazi wa kampuni hiyo katika kipindi cha saa 48 zilizopita
Image caption Kisa hicho kinafuatia shinikizo za serikali kwa wafanyikazi wa kampuni hiyo katika kipindi cha saa 48 zilizopita

Afisa mmoja wa kampuni ya uchimbaji madini kutoka Canada Acacia alizuiliwa kwa muda nchini Tanzania alipouwa akijaribu kulitoroka taifa hilo , kampuni hiyo iemsema katika taarifa.

Taarifa hiyo imesema kuwa afisa huyo mwandamizi alizuiliwa kwa muda huku cheti chake cha pasipoti kikihukuliwa katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.

Kisa hicho kinafuatia shinikizo za serikali kwa wafanyikazi wa kampuni hiyo katika kipindi cha saa 48 zilizopita, taarifa ilisema.

Mapema wiki hii Acacia ilisema katika taarifa kwamba serikali iliiambia kwamba inafaa kuilipa Tanzania dola bilioni 190 kupitia kodi, adhabu na riba.

Kampuni hiyo imekana na imechapisha habari hizo katika mtandao wake ili kupinga madai hayo.

Mada zinazohusiana