Polisi watibua njama ya magaidi kuangusha ndege Australia

Police man a check point in the Sydney inner suburb of Surry Hills on July 29, 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi watibua njama ya magaidi kuangusha ndege Australia

Polisi nchini Australia wametibua mipango ya kundi la magaidi ya kutaka kuangusha ndege, kulingana na Waziri Mkuu Malcolm Turnbull.

Majasusi wa Australia wanasema kuwa walipata habari kuwa watu hao walikuwa na njama ya kutumia mabomu ya kujitengenezea nyumbani.

Waziri Mkuu Malcolm Turnbull alisema kuwa mpango huo umevurugwa katika oparesheni kali iliyofanywa na kikosi maalumu cha kukabiliana na magaidi nchini.

Watu wanne wametiwa mbaroni kufuatia misako iliyofanywa kote katika mji wa Sydney na maafisa wa polisi waliojihami wakishirikiana na majasusi.

Mwanamke anayesema mumewe na mwanawe ni baadhi ya waliotiwa mbaroni amekanusha kuwa jamaa zake wanahusika na kundi lo lote la watu wa imani kali.

Usalama umeimarishwa katika uwanja wa ndege wa mji wa Sydney na kuenezwa katika maeneo mengine ya nchi.

Bwana Turnbull ametoa wito kwa wasafiri wa angani wawe watulivu na kuwa wanapaswa kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Hali ya hatari ya kukabiliana na magaidi nchini Australia ingali katika hali ya kawaida.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi watibua njama ya magaidi kuangusha ndege Australia

Mada zinazohusiana