Trump aikosoa China kwa kutoichukulia hatua Korea Kaskazini

People watch coverage of an ICBM missile test on a screen in a public square in Pyongyang on July 29, 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump aikosoa China kwa kutoichukulia hatua Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump amekosoa Uchina kwa kukosa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa Korea Kaskazini inasitisha mipango yake ya silaha za nukia.

Maoni yake yamechapishwa kwenye mtandao wa twitter siku moja baada ya Korea Kaskazini kufyatia kombora lake la pili linaloweza kusafiri kutoka bara moja hadi jingine mara ya pili chini ya muda wa mwezi mmoja.

Korea Kaskazini baadaye ilidai kuwa jaribio hilo linaonyesha kuwa silaha zake zinaweza kuishambulia Marekani.

Bwana Trump alisema amesikitishwa sana na Uchina na kuapa kuwa hataruhusu hali hii kuendelea.

Mnamo Jumamosi Uchina ilieleza masikitiko yake makubwa kuhusiana na kufyatuliwa kwa kombora hilo Korea Kaskazini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kim Jong-un akisherehekea jaribio la kombora

Mada zinazohusiana