Polisi wamuua mtu aliyeshambulia nyumbani mwa naibu wa rais Kenya

Ruto's home in Sugoi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mr Ruto's home in Sugoi village near the city of Eldoret

Polisi nchini Kenya wamemuuwa kwa kumpiga risasi mshambuliaji ambaye aliingia kwa nguvu makoa ya naibu wa rais nchini Kenya Willliam Ruto.

Bwana Ruto na familia yaka hawakuwa nyumbani humo katika kijiji kilicho karibu na mji wa Eldoret.

Mwanamume huyo aliingia nyumbani kwa naibu rais baada ya kumjeruhi mlinzi wa mlango kwa upanga na kumnyanganya bunduki ayke, kwa mujibu wa polisi.

Kisa hicho kinatokea siku chache kabla ya Kenya kuandaa uchaguzi wa Rais.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption William Ruto alikuwa ameindoka nyumbani kabla ya shambulizi

Mkuu wa polisi Joseph Boinet aliviambia vyombo vya habari kuwa hali sasa imedhibitiwa.

"Hakuna tisho sasa kwa sababu alikuwa ndiye peke yake"

Hakuna taafa zaidi iliyotolewa kuhusu shambulia hilo.

Ripoti za awali zilisema kuwa watu kadhaa waliokuwa wamejihami waliingi nyumbani mwa Ruto lakini badaye polisi wakasema kuwa alikuwa ni mshambuliaji mmoja tu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mr Ruto's home in Sugoi village near the city of Eldoret

Kumekuwa na ripoti za kukamnganya kuhusu ni bunduki ngapi mtu hiyo alitumia.

Bwana Boinet aliiambia radio moja kuwa ni mbunduki moja iliyokuwa ya mlinzi na imepatikana kutoka kwa mshambuliaji huyo.

Hata hivyo kamishina eneo la Ponde la Ufa Wanyama Musiambo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mshambuliaji alitumia bunduki kadha baada ya kuvuja na kuingia ghala la polisi lili ndani ya makao hayo na naibu Rais.

Image caption Kenya

Mada zinazohusiana