Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 30.07.2017 na Salim Kikeke

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Neymar

Baba yake Neymar ameiomba PSG kusubiri kuanza mazungumzo rasmi ya uhamisho wa pauni milioni 450 wa mwanae hadi baada ya Julai 31, tarehe ambayo atapata bakshishi yake ya pauni milioni 23.3 kutoka Barcelona ya kumshawishi Neymar kusaini mkataba mpya mwaka jana Oktoba. (Sunday Times)

Barcelona watawashtaki Paris Saint-Germain kwa UEFA kwa kukiuka kanuni za fedha (FFP) iwapo PSG watatoa dau la pauni milioni 197 kutengua kifungu cha usajili cha Neymar. (ESPN)

Iwapo Neymar, 25, ataondoka Barcelona na kujiunga na PSG, Barca huenda wakaamua kumchukua mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoinne Griezmann, 26 kuziba pengo. (Marca)

PSG wakikamilisha usajili wa Neymar, watapanda dau la pauni milioni 35 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 28 kutoka Arsenal. (Sunday Express)

Philippe Coutinho, 25, atamuomba meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kumruhusu ajiunge na Barcelona. Iwapo Coutinho ataondoka, Klopp atataka kumsajili winga wa Borussia Dortmund Christian Pulisic. (Sunday Mirror)

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Philippe Coutinho, 25, atamuomba meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kumruhusu ajiunge na Barcelona

Meneja wa RB Leipzig amesema kiungo Naby Keita, 22, anayenyatiwa na Liverpool ana asilimia 100 ya kubakia katika klabu hiyo ya Bundesliga. (Observer)

Uhamisho wa kiungo Nemanja Matic, 28, kutoka Chelsea kwenda Manchester United umekwama kutokana na kutofautiana kuhusu malipo ya marupurupu kwa Chelsea katika sehemu ya mkataba huo. (Sun on Sunday)

Manchester United huenda wakakamilisha usajili wa Nemanja Matic, 28, kutoka Chelsea mwishoni mwa wiki ijayo. (Daily Mail)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho atasubiri hadi msimu ujao kutoa pauni milioni 90 kumsajili Gareth Bale, 28, kutoka Real Madrid. (Sunday Express)

Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti "anapinga vikali" hatua ya kuondoka kwa winga Ivan Perisic, 28, ambaye amehusishwa na Manchester United. (Observer)

Manchester United wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 48 wa Ivan Perisic kutoka Inter Milan. (Daily Star)

Image caption Alexis Sanchez

Kiungo wa Manchester United Marouanne Fellaini, 29, amekubali mkataba wa kujiunga na Galatasaray ya Uturuki. (Ajansspor)

Manchester United wamehusishwa na kumtaka kiungo wa Anderlecht Leander Dendocker, 22, huku mkurugenzi wa klabu hiyo akisema timu ikija na dau la euro milioni 25-35, itakuwa vigumu kukataa. (Het Belang van Limburg)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, yuko tayari kuwasilisha maombi ya rasmi ya uhamisho ili kulazimisha uhamisho wake kwenda Manchester City. (Sunday Mirror)

Manchester City wamerejea katika orodha ya UEFA ya timu zinazomulikwa kwa kukiuka kifungu cha fedha (FFP) baada ya kutumia pauni milioni 220 kusajili msimu huu. (Sunday Telegraph)

Kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, anawindwa na timu sita za EPL, huku Tottenham na Manchester City wakiongoza mbio za kutaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Daily Star Sunday)

Everton wanafikiria kutoa pauni milioni 9 kumsajili beki wa West ham Winston Reid. (Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Chelsea Antonio Conte

Chelsea wapo tayari kutoa hadi euro milioni 70 kumsajili Alex Sandro. (Calciomercato)

Mkurugenzi wa michezo wa Roma, Monci, anasema klabu yake sasa inatazama kwingine baada ya dau jingine la kumtaka Riyad Mahrez, 26, kukataliwa na Leicester. (Evening Standard)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte atatoa ombi jipya kwa klabu la kununua wachezaji wapya zaidi wiki ijayo baada ya kusema ana wasiwasi wa kufukuzwa kazi. Tayari Chelsea wametumia pauni milioni 130 msimu huu. (Sunday Telegraph)

Newcastle wanataka kumsajili Lucas Perez, 28, wa Arsenal na kumfanya kuwa mshambuliaji mkuu wa klabu hiyo, licha ya mchezaji huyo kutaka kurejea katika klabu yake ya zamani Deportivo La Coruna. (Sun on Sunday)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.