Meya auawa wakati wa oparesheni ya madawa ya kulevya Ufilipino

Philippine President Rodrigo Duterte at a press conference shortly after arriving from Singapore at Davao international airport in southern island of Mindanao, 17 December 2016 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rodrigo Duterte

Meya wa mji mmoja wa Ufilipino, ambaye anatuhumiwa na Rais Rodrigo Duterte, kwamba amehusika na biashara ya mihadarati, ameuwawa katika msako wa polisi.

Reynaldo Parojinog, meya wa mji wa Ozamiz alipigwa risasi na kuuwawa, pamoja na mkewe na watu wengine 10, pale nyumba yake ilipovamiwa.

Polisi wanasema, walikuwa wakisaka katika nyumba hiyo, kukabidhi waranti ya kumkamata mtu ndipo utumiaji nguvu ukazuka.

Watu karibu elfu 9 wameuliwa katika misako ya polisi, au wameuliwa na magenge ya wanamgambo, tangu Rais Duterte kuingia madarakani mwaka jana, kufuatia kampeni ya uchaguzi, ambapo aliahidi kuua maelfu ya watu ili kufyeka biashara ya mihadarati nchini Ufilipino.

Polisi walipata bundukia, pesa na madawa ya kulevya kwa mujibu wa mkuu wa polisi Jaysen De Guzman.

Bwana Porojinog ndiye meya wa watata kuuliwa katika harakati kali za serikali kukabiana na madawa ya kelevya, ambapo bwana Duterte amewataja maafisa, polisi na majaji.

Hatua hiyo imempa umaarufu miongoni mwa wafilipino lakini imekoselewa na makundi ya kupigania haki za binadamu.

Image caption Ufilipino