Mahakama yakataa rufaa ya mwanajeshi wa Israel aliyemuua mpalestina

Israeli soldier Elor Azaria (C), who shot dead a wounded Palestinian assailant in March 2016, stands next to his mother Oshra (L) and father Charlie - 30 July 2017 Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Elor Azaria alikuwa mahakamani na wazazi wake Oshra na Charlie

Mahakama ya kijeshi ya nchini Israel, imekataa rufaa ya mwanajeshi, aliyepinga hukumu aliyopewa ya mauaji yasiyokusudiwa, baada ya kumpiga risasi na kumuua mshambuliaji ambaye alikuwa tayari amejeruhiwa.

Mahakama imekataa rufaa ya Elor Azaria ya kupinga hukumu aliyopewa ya kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela.

Kisa hicho kilitokea mwaka 2016, mjini Hebron katika eneo linalokaliwa, na tukio hilo lilinaswa katika video.

Video hiyo imeonyesha Azaria akimpiga risasi na kumuua Mpalestina aliyejeruhiwa bila ya Mpalestina huyo kuonyesha hasama yoyote kwa Azaria.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Maandamano yalifanyika dhidi ya Azaria

Mada zinazohusiana