Meneja wa teknolojia wa tume ya uchaguzi Kenya atoweka

Mwenyekiti wa IEBC nchini Kenya Wafula Chebukati Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwenyekiti wa IEBC nchini Kenya Wafula Chebukati

Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, imesema kuwa mmoja wa mameneja wake wa masuala ya teknolojia hajulikani aliko.

IEBC inasema kuwa mtu huyo alionekana mara ya mwisho siku ya Ijumaa jioni.

Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa mtu huyo aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS na mmoja wa wafanyakazi wenzake.

Aliyoandika kwenye ujumbe huo yalionyesha kuwa alikuwa akijielewa na alikuwa na mipango ya siku.

Ripoti tayari imepelekwa kwa polisi huku IEBC, familia yake na pia polisi wakishirikiana kujaribu kubainia aliko.

Kisa hiki kinatokea ikiwa imesalia juma moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Kenya ambao utafanyika tarehe 8 Agosti.