Matokeo ya kura yatarajiwa kutangazwa Senegal

Rais wa zamani Abdoulaye Wade 91 anawania tena Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa zamani Abdoulaye Wade 91 anawania tena

Kura zimekwishapigwa nchini Senegal huku televisheni ya umma ikiripoti kuwa asilimia 54 ya raia wa nchi hiyo wamejitokeza kupiga kura.

Rais wa zamani wa nchi hiyo, Abdoulaye Wade, amemshutumu rais wa sasa anayewaniwa muhula mwingine, Rais Macky Sall, kwa wizi wa kura, akisema kuwa baadhi ya maeneo yalikuwa bado hayajapokea karatasi za kupigia kura.

Polisi imesema wajumbe watatu wa muungano wa Bwana Wade walikamatwa kwa kufanya vurugu kwenye vituo vya kupigia kura.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Sall anatafuta wingi wa viti katika chama chake.

Rais Sall anatafuta wingi wa viti katika chama chake.

Abdoulaye Wade amethibitisha kuwa muunngano wa vyama vidogo vidogo unamuandaa mtoto wake wa kiume Karim kuwania urais mnamo mwaka 2019.

Mgombea mwingine ni meya wa mji mkuu wa Senegal , Dakar, ambaye yuko gerezani kwa mashtaka ya ubadhilifu wa mali ya umma.

Matokeo ya awali yanatarajiwa kutangazwa Jumatatu asubuhi.

Mada zinazohusiana