Marekani: Muda wa mazungumzo kuhusu Korea Kaskazini umekwisha

Huwezi kusikiliza tena
The US B-1 bombers were joined by South Korean and Japanese planes

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe anasema yeye pamoja na rais wa Marekani Donald Trump wamekubaliana kuwa upo umuhimu wa kupambana na Korea ya Kaskazini katika mipango yake ya majaribio ya makombora.

Abe amewaambia waandishi wa habari kuwa anashukuru kujitolea kwa Rais Trump katika suala la Korea ya Kaskazini.

Mapema Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley alisema muda wa mazungumzo umemalizika.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mapema Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley alisema muda wa mazungumzo umemalizika.

Haley amesema hakuna sababu ya kuwa na kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iwapo hakutakuwa na matokeo, yatakayoipa mbinyo Korea Kaskazini na China ni lazima iamue kama itaamua kuchukua hatua hii muhimu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Korea kaskazini kufanya jaribio lingine la makombora yake siku ya Ijumaa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marekani imesema kuwa mtambo wake wa kuangusha makombora wa Thaad umefanikiwa
Image caption Mchoro wa kuonyesha uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini
Image caption Jingi mfumo wa Thaad unafanya kazi
Image caption Thaad