Shambulio lawaua watu 6 Mogadishu

Shambulio lawaua watu 6 Mogadishu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shambulio lawaua watu 6 Mogadishu

Watu sita wameuawa katika mlipuko wa bomu mjini Mogadishu Somalia na wengine 10 wamejeruhiwa.

Katika tukio jingine kusini magharibi mwa Mogadishu, wapiganaji wa Al Shabaab wanadai kuwaua maafisa wengi wa kikosi cha muungano wa Afrika - AMISOM.

Msemaji wa kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia (AMISOM) amethibitisha kuwepo mapigano lakini haukubaini ni wanajeshi wangapi wameuawa au kujeruhiwa.

Bomu la kutegwa ndani ya gari lililipuka dakika chache nje ya maduka dakika chache baada ya saa tano katika mtaa wenye shughuli nyingi katika mji huo mkuu.

Walioshuhudia wanasema ulikuwa mlipuko mkubwa sana na kwamba watu wengi walikufa ama kujeruhiwa.

Mashambulio haya yanakuja baada ya wiki kadhaa za utulivu katika mji mkuu Mogadishu kufuatia mashambulio ya hapa na pale ya kundi la Al-Shabaab.

Katika tukio jingine tofauti vikosi vya Muungano wa Afrika vilikabiliana na wanamgambo wa Alshaabab katika mkoa wa Lower Shabelle yapata kilomita 140 kusini magharibi mwa mji huo mkuu.

Kundi la Al-Shabaab limesema liliwauwa askari 39 katika shambulio la kuvizia, lakini idadi hiyo haijathibitishwa na vyanzo huhu vya habari.