Cristiano Ronaldo kufika mahakamani kujibu mashtaka ya kukwepa kodi

Real Madrid's Portuguese forward Cristiano Ronaldo pictured on 2 June, 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 ni mwanasoka wa hivi punde kuchunguzwa na mamlaka za kukusanya ushuru nchini Uhispania

Cristiano Ronaldo anatarajiwa kufika mahakamani nchini Uhisipania leo baada ya kulaumiwa kwa kukwepa kulipa kodi.

Waendesha mashtaka wanadai kuwa Ronaldo ambaye ni mcheza soka anayeripotiwa kulipwa fedha nyingi zaidi duniani, alikwepa kulipa kodi ya dola milioni 17.3 tangu mwaka 2010.

Nyota huyo wa Real Madrid amekana madai hayo.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 32 ni mwanasoka wa hivi punde kuchunguzwa na mamlaka za kukusanya ushuru nchini Uhispania.

Muargentina Lionel Messi ambaye anachezea klabu ya Barcelona, alihukumiwa kifungo cha miezi 21 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa kama hayo mwaka uliopita.

Mapema mwaka huu mahakama iliamua kuwa atalipa Euro 232,000 badala ya kufungwa

Hata hivyo Messi alilaumiwa kwa kutolipa Euro milioni 4.1 tu chini ya zile Ronald anadaiwa na atatoa ushahidi mahakamani mjini Madrid leo Jumatatu.