Uchaguzi Kenya: Nilikimbia nikauacha mkono wangu nyuma

Uchaguzi Kenya: Nilikimbia nikauacha mkono wangu nyuma

DJ One Hand alikuwa katika mtaa wa Mathare, jijini Nairobi ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 zilipozuka.

Aliona kundi la watu likimzingira mwanamke na akadhamiria kumsaidia mwanamke huyo.

Hakujua kwamba wapo wengine waliokuwa wanamtazama na ghafla alishtukia amekatwa mkono wake mmoja.

Alilazimika kukimbilia usalama wake.

Ana ujumbe gani uchaguzi mkuu Kenya unapokaribia?