Mungu huzungumza kupitia kwangu adai mfalme wa Zulu

Mungu huzungumza kupitia kwangu adai mfalme wa Zulu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma (kushoto) mfalme wa Zulu (kulia)

Mfalme mwenye ushawishi mkubwa nchini Afrika Kusini wa jamii ya Zulu Goodwill Zwelithini, anasema wakati mwingine Mungu humzungumzia na lazima aseme lile Mungu amesema kwa wananchi.

Mfamle aliyesema hayo wakati wa shereha za kufana zilizofanyika siku Jumamosi eneo la Nongoma, kitovu cha ufalme wake katika mkoa wa KwaZulu-Natal kama sehemu ya sherehe za kuadhimisha siku yake kuzaliwa anapohitimu miaka 69.

Alipewa zawadi ikiwemo mvinyo, ng'ombe na farasi.

Mfalme mteule wa Thailand kuthibitishwa Desemba

Mfalme wa Japan aomba kung’atuka

Mfalme wa Thailand kuombolezwa mwaka mmoja

Alinukuliwa akisema, "Wakati mwingine nikiongea, sio mimi ninaongea lakini mtu huzungumzia kupitia kwangu. Ninaamrishwa na ni lazima niyaseme upende usipende.

Kulingana na mtandao wa habari wa IOL, alisema kuwa wakati mwingine Mungu aliuamuambia kuwaombea watu fulani na kuwawekea mikono ili kuwaponya.

Hata kuzaliwa kwangu kulikuwa tofauti, kulitabiriwa.

Mada zinazohusiana