Wanafunzi 36 wa Zambia wakwama India

Vitabu

Wanafunzi zaidi ya 36 raia wa Zambia wamekwama nchini India baada ya kukosa kupewa idhini ya kuondoka na vyuo vikuu walivyokuwa wakisomea.

Balozi wa Zambia nchini India Judith Kapijimpanga, amesema wengi wao wamekwama baada ya kushindwa kumaliza kulipa karo ya chuo.

Wengine walifeli kwenye mitihani yao lakini wameshindwa kuwafahamisha wazazi wao kuhusu hilo.

Bi Kapijimpanga amesema baadhi ya wanafunzi walifanya uhalifu, baadhi wakipatikana na makosa kama vile matumizi ya madawa ya kulevya.

Serikali ya Zambia inapanga kushauriana na wizara ya mambo ya nje kuhakikisha wanafunzi hao wanarejea nyumbani, balozi huyo amesema.

Mada zinazohusiana