Qatar yawasilisha malalamishi kwa WTO

Qatar imewasilisha malalamiko rasmi katika Shirika la Kimataifa Biashara WTO dhidi ya vikwazo vya kiuchumi vilivyoweka dhidi yake mwezi June na nchi za kiarabu ambazo ni majirani zake. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Qatar imewasilisha malalamiko rasmi katika Shirika la Kimataifa Biashara WTO dhidi ya vikwazo vya kiuchumi vilivyoweka dhidi yake mwezi June na nchi za kiarabu ambazo ni majirani zake.

Qatar imewasilisha malalamiko rasmi katika Shirika la Kimataifa Biashara WTO dhidi ya vikwazo vya kiuchumi vilivyoweka dhidi yake mwezi June na nchi za kiarabu ambazo ni majirani zake.

Waziri wa uchumi na biashara wa Qatar Sheikh Ahmed bin Jassem bin Mohammed Al Thani amesema vikwazo hivyo vya kiuchumi vilivyoongozwa na Saudia Arabia vimekiuka moja kwa moja sheria za biashara za kimataifa.

Nchi za kiarabu ambazo ziliweka vikwazo hivyo kwa sasa zitakuwa na siku 60 kumaliza mgogoro huo.

Nchi hizo za kiarabu bado hazijajibu rasmi malalamiko hayo, lakini hata hivyo umoja huo walishawahi kusema WTO wanapaswa kuangalia maswala ya usalama wa taifa ili kupata uhalali wa kuichukulia hatua nchi ya Qatar.