Mwizi apatikana amelewa ndani ya nyumba aliovunja

Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani. Haki miliki ya picha ESPERANCE POLICE
Image caption Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani.

Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani .

Polisi wanasema jamaa huyo wa miaka 36 alivunja na kuingia nyumbani humo mjini Esperence , magharibi mwa Australia siku ya Ijumaa.

Alilewa baada ya kunywa kinywaji hicho ,kulingana na maafisa.

Mwenye nyumba hiyo alirudi nyumbani na kumpata mwizi huyo amelala kitandani mwake.

''Alitoka nje na kuwapigia simu polisi ambao waliwasili na kumkamata mshtakiwa'', alisema sajenti Richard Moore kutoka polisi ya Esperence .

Mtu huyo alipelekwa hospitalini baada ya kupatikana amelewa chakari alisema sajenti Moore.

Ameshtakiwa na wizi.