Diamond ampeleka mkewe Mombasa kumliwaza

Msanii wa Tanzania Diamond
Image caption Msanii wa Tanzania Diamond

Mwimbaji maarufu nchini Tanzania Diamond Platinumz na mkewe Zari Hassan wako katika likizo mjini Mombasa nchini Kenya.

Wawili hao waliingia katika hoteli ya kifahari ya English Point Marina mjini humo kwa likizo ya siku tano kulingana na gazeti la Daily Nation nchini Kenya.

Katika ukurasa wake wa Instagram , Diamond ambaye jina lake kamili ni Naseeb Abdul alisema kuwa likizo hiyo inalenga kumliwaza mkewe baada ya kumpoteza mamake Halima Hassan.Wanaandama na meneja wa Diamond katikja mji huo wa kitalii.

" Mtoto wa watu katoka kwenye matatizo mfululizo msijifanye ni tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie nyumbani… Nina siku 5 za kumpetipeti ; leo ndio kwanza'', alichapisha Diamond katika ukurasa wake wa Instagram.

Hii ni baada ya Zari kukosolewa na baadhi ya mashabiki kwa kutotumia wakati wake akimuomboleza mamake na mumewe wa zamani Ivan Ssemwanga.

Siku ya Jumamosi mwimbaji huyo wa Eneka, alisamabaza picha na video katika mtandao wake wa Instagram akiwa na mkewe Zari Hassan wakijishebedua.

Mada zinazohusiana