China yafungua kambi yake ya kijeshi Djibouti

China hatimaye imefungua rasmi kambi yake ya kijeshi katika taifa la Djibouti siku ya Jumanne kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Image caption China hatimaye imefungua rasmi kambi yake ya kijeshi katika taifa la Djibouti siku ya Jumanne kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

China hatimaye imefungua rasmi kambi yake ya kijeshi katika taifa la Djibouti siku ya Jumanne kulingana na chombo cha habari cha Reuters.

China ilianza ujenzi wa kituo hicho cha mipango nchini Djibouti mwaka uliopita.

Kitatumika kusambaza meli za wanamaji wake wanaoshiriki katika maswala ya kulinda amani na mipango ya kibinaadamu katika pwani ya Yemen na hususan Somalia, Reuters imeongezea.

Ni kambi ya kwanza ya wanamaji katika taifa la kigeni ,ijapokuwa maafisa wa Beijing wameitaja kuwa eneo la kupanga mikakati , Reuters imenukuu vyombo vya habari nchini humo vikisema.

Ripoti hiyo imesema kuwa kambi hiyo itasaidia China kuimarisha doria zake katika maji yasio ya Somalia na Yemen mbali na kutekeleza majukumu yake ya kibinaadamu.

Hata ijapokuwa Djibouti ni nchi ndogo, ina kambi za kijeshi za Marekani na Ufaransa.

Mada zinazohusiana