Aliko Dangote aombwa kukamilisha ujenzi wa kiwanda kikubwa zaidi cha mafuta duniani

Aliko Dangote Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliko Dangote

Mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote, ameombwa na serikali ya Nigeria kukamilisha ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta mapema ya muda wake rasmi wa kukamilika mwaka 2019.

Gazeti la Premium Times la nchini Nigeria lilimnukuu waziri wa mafuta Ibe Kachikwu akisema, "Rais Buhari angependa kupata kuwa anakuja kukifungua kiwanda kikubwa kama hiki kabla ya muhula wake kukamilika"

"Ninaona tarehe ya kukamilika ujenzi wa kiwanda hiki ni Disemba mwaka 2019, lakini ninajua unaweza kuelewa kuwa ningependa mradi huu kukamilika mapema kuliko ulivyopangwa," waziri alinukuliwa akimuambia Dangote alipotembelea mradi huo mjini Lagos.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uhaba wa mafuta huikumba Nigeria mara kwa mara

Kiwanda hicho ndicho kikubwa zaidi cha kusafisha mafuta duniani kilichojengwa eneo moja na cha pili kwa kutengeneza mbolea duniani.

Licha ya kuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa zaidi wa mafuta duniani, Nigeria hununua asilimia kubwa ya mafuta kutoka nje na kwa sasa inakabiliwa na uhaba mkubwa.

Wakati ujenzi wa kiwanda hicho utakamilika kitakuwa na uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 kwa siku kwenda petroli, gesi ,mafuta ya taa na ya ndege.

Image caption Wakati mwingine watu hulazimika kusubiri kupata mafuta

Mada zinazohusiana