Polisi wagundua madhabahu ya dhehebu linalowaua watu Nigeria

Wanachama wa dhehebu la Badoo wanatajwa kuwa washukiwa wa mauaji wa watu wanne wa familia moja yaliyotokea katika kijiji hicho siku ya Jumapili Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanachama wa dhehebu la Badoo wanatajwa kuwa washukiwa wa mauaji wa watu wanne wa familia moja yaliyotokea katika kijiji hicho siku ya Jumapili

Polisi mjini Lagos nchini Nigeria wanasema kuwa wamegundua madhabahu yanayomilikiwa na watu wanashukiwa kuwa wanachama wa dhehebu linalojulikana na Badoo

Polisi waligundua makaburi na vifaa vya kutoa kafara katika kijiji cha Ikorodu mjini Lagos kwa mujibu wa gazeti la Vanguard ambalo pia liliripoti kuwa wanachama wanne wa kundi hilo walikamatwa.

Wanachama wa dhehebu la Badoo wanatajwa kuwa washukiwa wa mauaji wa watu wanne wa familia moja yaliyotokea katika kijiji hicho siku ya Jumapili

Licha ya kuthibitisha kukamatwa watu hao, polisi bado hawajatoa taarifa rasmi kuhusu uchunguzi unaoendelea.

Mada zinazohusiana