Wabunge wamchagua waziri mkuu mpya Pakistan

Shahid Khaqan Abbasi leaves after submitting his nomination paper at the National Assembly (lower house of the parliament) in Islamabad, Pakistan, 31 July 2017 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bwana Abbasi alichaguliwa kwa kura 221 kati ya kura 342 za wabunge.

Wabunge nchini Pakistan wamemchagua Shahid Khaqan Abbasi kuwa waziri mkuu mpya kuchukua mahala pake Nawaz Sharif, ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita kufuatia madai ya ufisadi.

Chama kinachotawala kinamtaka waziri huyo wa zamani wa mafuta kushika wadhifa huo kwa muda hadi pale ndugu yake bwana Sharif, Shahbaz Sharif atakapo chukua hatamu.

Shahbaz Sharif, kiongozi wa jimbo la Punjap ni lazima ashinde uchaguzi mdogo wa bunge kuweza kuhitimu kuwa waziri mkuu.

Bwana Abbasi alichaguliwa kwa kura 221 kati ya kura 342 za wabunge.

Alimshukuru Nawaz Sharif baada ya kuchaguliwa na kukana madai kuwa atahudumu kwa muda kabla ya kumuachia Sahbaz Sharif.

Makundi ya upinzani nayo yalikuwa na wagombea wao lakini chama tawala cha Pakistan Muslim League-Nawaz (PML-N) kina wingi wa wabunge na ilikuwa rahisi kwacho kupata ushindi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shahbaz Sharif, kiongozi wa jimbo la Punjap ni lazima ashinde uchaguzi mdogo wa bunge kuweza kuhitimu kuwa waziri mkuu.

Mada zinazohusiana