Ikulu ya Whitehouse yakiri Trump alimsaidia mwanawe kuandika taarifa ya mkutano wake

Trump na mwanawe Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Trump na mwanawe

Ikulu ya Whitehouse imethibtisha ripoti kwamba rais Donald Trump alimsaidia mwanawe kuandika taarifa ya mkutano wake na wakili wa Urusi mwaka uliopita.

Bwana Trump alipima majibu ya mwanawe kwa vyombo vya habari lakini hakumfunza maneno atakayosema, ikulu hiyo ilisema

Donald Trump Jr alisema mkutano huo ulikuwa kuhusu upangaji wa watoto nchini Urusi kabla ya kukiri kwamba alipewa habari mbaya dhidi ya Hillary Clinton.

Wakili wa rais awali alikuwa amekana kwamba rais Trump alitoa usaidizi wowote katika taarifa hiyo.

Mwana huyo mwenye umri wa miaka 39 alichunguzwa baada ya gazeti la New York Times kuanza kuripoti mwezi uliopita kuhusu mkutano wake wa mwezi Juni 2016 katika jumba la Trump Tower.

Msemaji wa Ikulu ya Whitehouse Sarah Huckabee Sanders aliambia vyombo vya habari siku ya Jumanne.

''Rais alipima uzito wa taarifa hiyo kama baba yeyote yule'' .

Mada zinazohusiana