Nyumba ya rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan yaporwa Abuja

Nyumba ya Goodluck Jonathan yaporwa Abuja Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nyumba ya Goodluck Jonathan yaporwa Abuja

Nyumba ya rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan kwenye mji mkuu Abuja, imeporwa na wezi kwa mujibu wa msemaji wake aliyenukuliwa na gazeti la Premium Times.

Ikechuku Eze alisema kwa wizi huo ulifanyika mwezi uliopita.

Alisema kuwa wezi hao waliiba kila kitu vikiwemo viti, vitanda, vifaa vya elektroniki na vitu vingine vingi na hata milango ya vyumba vya ndani.

Lakini hata hivyo alikana madai kuwa televishi 36 na jokofu 25 ziliibiwa.

Alisema kuw ni televiseni 6 na jokofu 3 zilizoibiwa. Washukiwa kadha wakiwemo polisi sita wamekamatwa.

Mada zinazohusiana