Usain Bolt amtaja Wayde van Niekerk kama mrithi wake

Wayde van Niekerk(kushoto) Usain Bolt(kulia) Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wayde van Niekerk(kushoto) Usain Bolt(kulia)

Mwanariadha wa Afrika Kusini Wayde van Niekerk, anatarajiwa kuchukua usukani kama mwanariadha nyota duniani baada ya bingwa Usain Bolt kustaafu , kwa mujibu wa Bolt mwenyewe.

Bolt atastaafu kutoka riadha baada ya mashindano ya riadha ya ubingwa wa dunia ambayo yataanza jijini London siku ya Ijumaa.

Bolt amekuwa kivutio kikubwa cha riadha baada ya kushinda mbio za mita 100 na 200 mjini Beijing mwaka 2008.

"Van Nieker kwa kweli ameonyesha kuwa yeye ni nyota wa dunia." Bolt alijibu alipoulizwa na mwandishi wa BBC Dan Roan.

Van Niekerk alishinda dhahabu katika mbio za mita 400 kwenye mashindano ya mwaka uliopita ya olimpiki ya Rio kwa muda wa sekunde 43.03.

Mada zinazohusiana