Miili ya wanajeshi wa Uganda waliouawa Somalia yawasili nyumbani

Miili ya wanajeshi wa uganda yawasili nyumbani
Image caption Miili ya wanajeshi wa uganda yawasili nyumbani

Miili ya wanajeshi 12 wa Uganda waliouawa nchini Somalia siku ya Jumapili imesafirishwa nyumbani.

Shere ya kijeshi ilifanyika wakati miili hiyo iliwasili uwanja wa ndege wa Entebbe.

Familia zilifika na wengine walikuwa na husuni wakati ndege ilitua uwanjani.

Image caption Miili ya wanajeshi wa uganda yawasili nyumbani

Wanajeshi wa Uganda huchukua asilimia kubwa ya kikosi cha Amisom kinachoiunga mkono serikali ya Somalia katika vita dhidi ya al-Shabab.

Hao ndio wanajeshi wengi zaidi wa Uganda kuuliwa nchini Somalia tangu mwaka 2015 wakati wanajeshi 19 waliuliwa wakati wa shambulizi la al-Shabab.

Image caption Miili ya wanajeshi wa uganda yawasili nyumbani

Mada zinazohusiana