Itali kutuma meli za kuwazuia wahamiaji Libya

Wahamiaji wa Libya
Image caption Wahamiaji wa Libya

Bunge la Italia limeidhinisha mpango wa kutuma meli za kivita katika bahari ya Libya kusitisha wahamiaji kuvuka bahari ya Meditarenia.

Italy ndio taifa linalopokea wahamiaji wengi wanaosafiri kutoka Libya, nchi inayotumika na wahamiaji wengi wa kutoka kusini mwa jangwa la Sahara kuingia Ulaya.

Italia haitaki wahamiaji na wakimbizi zaidi wanaowasili nchini humo .

Kura ya hivi karibuni ya bunge iliashiria mwanzo wa mafanikio ya azma ya taifa hilo kuwasukuma nyuma wahamiaji na wakimbizi katikati mwa bahari ya Mediterranean.

Hilo lilidhihirika katika mipango ya awali ya wizara ya ulinzi ya kutuma meli mbili pekee ndani ya eneo la maji la Libya kusaidia walinzi wa mwambao wa Libya.

Lakini wataliano wanatumai kutuma meli nyengine zaidi pamoja na helikopta na ndege zisizokuwa na rubani kuchunguza biashara haramu ya kuwasafirisha watu baharini.

Makundi ya waangalizi wa haki za binadamu wanahofia kuwa hili litawafanya wahamiaji zaidi kukiuka sheria za uhamiaji ikiwa watarejeshwa Libya.

Mara kwa mara wahamiaji wanaohifadhiwa katika mazingira duni, hupigwa na hata kubakwa.