Raia wa Rwanda wanaoishi ng'ambo wapiga kura

Karani wa shughuli ya kupiga kura katika ubalozi wa Rwanda nchini Kenya
Image caption Karani wa shughuli ya kupiga kura katika ubalozi wa Rwanda nchini Kenya

Raia wa Rwanda wanaoishi nje ya taifa hilo wanashiriki katika uchaguzi wa uraisi hii leo kabla ya raia wa taifa hilo kushiriki rasmi katika shughuli hiyo siku ya Ijumaa nchini mwao.

Tayari raia wa Rwanda wanaoishi katika mataifa ya Afrika mashariki wameanza kushiriki katika uchaguzi huo.

Uchaguzi huo unashirikisha wagombea wakuu watatu

Rais wa Rwanda Paul Kagame ambaye ni miongoni mwa wagombea wakuu kupitia chama tawala cha RPF anawania kuongoza kwa muhula mwengine wa miaka saba mamlakani.

Haki miliki ya picha Empics
Image caption Raia wa Rwanda akishiriki katika shughuli ya kupiga kura nchini Kenya

Wapinzani wake wakuu ni Frank Habineza and Phillipe Mpayimana.

Mapema siku ya Alhamisi raia hao wa Rwanda walijaa katika vituo vya kupigia kura katika ubalozi wa Kenya, Tanzania na Uganda tayari kumchagua kioingozi wao.

Mbali na raia wanaoshi katika mataifa jirani, raia hao wanaoshi nchini Ufaransa, Ubelgiji ,Marekani na canada pia wanashiriki katika zoezi hilo.

Image caption Balozi wa Rwanda nchini Kenya James Kimonyo

Wengi walisafiri kutoka maeneo mbali mbali ya mataifa ya Afrika mashariki ili kushiriki katika zoezi hilo la kihistoria.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mwendo wa saa moja nchini Kenya, Uganda na Tanzania na milolongo mirefu ya wapiga kura ilishuhudiwa.

Mabasi, teksi na magari ya kibinafsi yalijaa katika balozi hizo za Rwanda wakati wa shughuli hiyo.

Image caption Shughuli ya kupiga kura

Kuna takriban vituo 98 vya kupigia kura mbali na wapiga kura zaidi ya 44,000 watakaoshiriki katika shughuli hiyo kwa raia wanaoishi nje ya taifa hilo.